CCM Kuazimisha miaka 40 Februry 5, Shamra shamra zaanza rasmi.

Chama cha mapinduzi CCM kinatarajia kuazimisha Miaka 40 ya kuzaliwa kwa chama hicho kwa kufanya shughuli mbali mbali za kijamii ikiwemo usafi wa mazingira na kuwafariji wagonjwa na wazee wasiojiweza.
Akizungumza na waandishi wa habari huko ofisini kwake Kisiwanduni Mjini Zanzibar Katibu wa Idara ya Itikadi na Uwenezi  CCM Waride Bakari Jabu amesema maadhimisho hayo pia yanatarajiwa kufanyika kwa ngazi mbalimbali kuazia shehia,Wilaya na Mikoa kwa wanachama kushiririki shughuli za kijamii zilizopangwa kufanyika pamoja na kushiriki Mikutano ya kamati za siasa.
Hata hivyo amesema katika kipindi cha miaka 40 ya CCM nchi inaendelea kuwa na mafanikio makubwa yanayotokana na uwepo wa amani ,pamoja na  kuendeleza muungano  wa Zanzibar na Tanzania bara  uliyokusudia na Kuinua shughuli za kiuchumi zilzopo.
Aidha ametoa wito kwa wanachama wa Chama cha mapinduzi CCM kuwa mstari wa mbele katika kushiriki shamramra za maadhimisho hayo yanayotarajiwa kuanzia hapo kesho na na kilele chake kumalizikia February5.

Comments