Bw. Adama Barrow ameapishwa kuwa rais wa Gambia kwenye ubalozi wa nchi hiyo mjini Dakar, Senegal. Akihutubia muda mfupi baada ya kuapishwa Bw Barrow aliwashukuru waungaji mkono wake ambao kwa mara ya kwanza wamechagua rais kwa kupiga kura, na kusema atarudi Gambia haraka iwezekanavyo na kuunda serikali.
Bw. Barrow alichaguliwa kuwa rais kwenye uchaguzi uliofanyika tarehe 2 Desemba mwaka jana, lakini hawezi kuchukua madaraka moja kwa moja kutokana na upinzani wa rais wa zamani Yahya Jammah.
chanzo: cri.
Comments