Biaharusi huyo mkaazi wa kivumoni Msuka Wilaya ya Micheweni,
alitoroka nyumbani kwao usiku wa manane kuamkia siku ya Jumatano siku
ambayo ilikua ifanyike harusi hiyo na hadi sasa hajulikani alipo.
Akizungumza na muandishi wa habari hizi bwana harusi Ali Khelef
alisema, tayari amepata hasara kubwa kutokana na maandalizi ya shughuli
hiyo kwa sababu ameshapokea jamaa zake kutoka sehemu mbalimbali hivyo
aliwaomba wanafamilia wa binti huyo kumtafuta ili shughuli hiyo
ikamilike.
Kwa upande wa familia ya bwana harusi wamesema bado hawajatoa maamuzi
juu ya suala hilo lakini wanatarajia kukutana pande zote mbili ili
kutoa maamuzi ya pamoja.
Kwa upande wa bi harusi mwandishi wa habari hizi hakupata ushirikiano
kutokana na kuambiwa kuwa baba wa familia hayupo na hajulikani atarudi
saa ngapi nyumbani.
Kwa upande wa majirani wamesikitiswa na kitendi hicho na kusema kua
iwapo upande wa bi harusi hawakukubaliana na suala hilo nivyema wangetoa
taarifa mapema kabla ya maandalizi.
Aidha taarifa ambazo zimepatikana kutoka kwa mmoja wa familia ya
bwana harusi zinasema iwapo watashindwa kukubaliana na upande wa
biharusi watafungua kesi ya madai wakidai kurejeshewa gharama
walizotumia kwa ajili ya harusi hiyo ambayo haikufanyika..
chanzo; zanzibar24.
Comments