Wapiganaji wanaomtii kiongozi wa
kijeshi, Jemedari mkuu Khalifa Hefter wamesema wamewaondoa wanamgambo wa
kiislamu katika wilaya ya Ganfouda.
Eneo hilo lilikuwa limezingirwa kwa miezi kadhaa na limeonekana kuwa na mapigano mabaya zaidi katika kuidhibiti Benghazi.
Baadhi ya wapiganaji wa kiislamu wana mafungamano na mtandao wa Al Qaeda.
Jemedari
mkuu Hefter aliongoza mapambano dhidi yao, ingawa jeshi lake
halitambuliwi na serikali ya Libya inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa.
chanzo:bbc.
Comments