Baraza la wawakilishi, Iran kushirikiana.

Zanzibar na Iran zinakusudia kutanua wigo wa Ushirikiano  katika masuala ya Kibunge ili kubadilishana uzowefu na  mbinu bora za kuendesha vyombo hivyo.

Makubaliana hayo yamefikiwa jana wakati wa Mazungumzo ya pamoja kati ya Spika wa Baraza la Wawakilishi Zubeir Ali Maulid  na Msaidizi Balozi Ofisi ya Ubalozi wa Iran Mohammad Dehghani.

 Makubaliano hayo yaliofikiwa katika Ofisi za Baraza la Wawakilishi Chukwani nje Kidogo ya Mji wa Zanzibar pia yamelenga kuwajengea uwezo wajumbe wa baraza la wawakilishi katika kuwatumikia wananchi.

Katika mazungumzo hayo viongozi hao pia wamekubaliana kuendelezwa kwa ushirikiano uliopo wa muda mrefu ili kuleta maslahi zaidi kwa nchi hizo mbili.

Ubalozi wa Iran hapa nchini kwa niaba ya Spika wa Bunge la Iran  amemuwalika rasmi spika Zubeir kutembelea bunge la nchi hiyo mwezi ujao.

chanzo; Zanzibar24

Comments