Alisema ziara hiyo ya Kiserikali ilimuwezesha na kumpa fursa ya
kukutana na Uongozi wa Kampuni na Taasisi mbali mbali za China
zilizoonyesha nia ya kutaka kuwekeza vitega uchumi vyao Visiwani
Zanzibar.
Balozi Seif Ali Iddi alieleza hayo hapo Ofisini kwake Vuga Mjini
Zanzibar wakati wa mazungumzo yake na Balozi Mdogo wa Jamuhuri ya Watu
wa China hapa Zanzibar Bwana Xie Xiaolon akimshukuru kwa kukamilisha
ziara hiyo kwa mafanikio makubwa.
Alisema Mikutano ya pamoja kati ya Ujumbe wa Zanzibar na Uongozi na
Makampuni mbali mbali waliyokutana nayo yalikuwa na muelekeo mwema wa
ushirikiano kati ya pande hizo mbili.
“ Ratiba yote iliyopangwa ndani ya ziara hiyo imetekelezwa kwa
asilimia kubwa na kuonyesha matumaini mapya ya ushirikiano na uhusiano
uliopo kati ya China na Zanzibar na Tanzania kwa ujumla”. Alisema Balozi
Seif.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alimueleza Balozi mdogo wa China
aliyepo Zanzibar kwamba Makampuni ya Umeme ya TBEA, Uvuvi ya Hongdong,
ile inayotoa huduma za Kijamii ya Avic pamoja na Kampuni ya MCC –
Oversease tayari wataalamu wake wameshaangalia mazingira ya Zanzibar na
kujiandaa namna ya kuanzisha miradi yao Zanzibar.
Naye Balozi Mdogo wa Jamuhuri ya Watu wa China Bwana Xie Xiaolon
alisema Zanzibar na China daima zitaendelea kushirikiana katika njia ya
uanzishwaji wa miradi ya pamoja itakayosaidia kuleta ustawi wa wananchi
wa sehemu hizo mbili.
Bwana Xie alimuhakikishia Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwamba
juhudi zitaendelea kuchukuliwa katika kuona miradi ya maendeleo
iliyoanzishwa kupitia msaada au udhamini wa Serikali ya China
itatekelezwa na kukamilika kama ilivyokusidiwa.
chanz; zanzibar24.
Comments