Alisema Serikali Kuu kazi yake kubwa ni kuongeza nguvu za uwezeshaji
katika kuona miradi hiyo inaimarika na kukua kwa lengo la kuwaondoshea
ukali wa maisha Wananchi wake katika maeneo mbali mbali ya Visiwa vya
Unguja na Pemba.
Unguja na Pemba.
Balozi Seif Ali Iddi alisema hayo akiwa katika ziara ya siku Tatuni
Kisiwani Pemba kuangalia miradi ya Maendeleo wakati alipokagua miradi ya
Tasaf katika Bonde la Kidau Ndagoni kuona maendeleo ya ujenzi wa Tuta
la kuzuia maji ya Bahari yanayoathiri wakulima wa bonde hilo.
Alisema yapo maendeleo makubwa yaliyopatikana tokea kuanzishwa kwa
Mfuko wa Maendeleo ya Jamii Tanzania {TASAF} hasa katika kuzisaidia Kaya
Maskini zilizozongwa na ukali wa maisha ziwe na miundombinu ya
kujiendesha Kimaisha kupitia miradi wanayoianzisha.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwapongeza Wananchi na wakulima
hao wa Bonde la Kidau pamoja na wale wote wanaopata huduma kupitia mfuko
wa Tasaf kutokana na juhudi kubwa wanazozichukuwa katika kuimarisha
miradi yao ikiwemo ile ya sekta ya kilimo iliyokuwa tegemeo kubwa la
wananchi wa Zanzibar kwa zaidi ya asilimia 8%.
Akitoa ufafanuzi wa kitaalamu wa ujenzi wa Tuta hilo la kuzuia maji
ya bahari katika Bonde la Kidau Ndagoni Mhandisi wa Wizra ya Kilimo,
Maliasili, Mifugo na Uvuvi nd. Talib Bakari alisema zaidi ya Eka 33
kwenye Bonde hilo zimekuwa zikiingia Maji ya Bahari.
Nd. Bakari alisema hali hiyo imewafanya Wakulima wapatao 92
wameathirika na tatizo hilo lililopelekea kukosa kuendelea na harakati
zao za kilimo cha Munga pamoja na mazao mengine ya nafaka.
Mhandisi Bakari alimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwamba
athari hiyo iliyokuwa kero kwa wakulima hao na pia kuchangia uharibifu
wa mazingira ilipeklekea wananchi na Wakulima hao kuwamua ujenzi wa
Tuta ili kunusuru hali hiyo.
Tuta ili kunusuru hali hiyo.
Alisema ujenzi wa Tuta hilo la kuzuia maji ya Bahari ambao kwa sasa
umeshafikia asilimia 90% unaotarajiwa kuchukuwa siku 45 hadi kukamilika
kwake utaweza kuwafaidisha Wakulima 92.
Alifafanua kwamba gharama za ujenzi wa Tuta hilo utafikia jumla ya
shilingi Milioni 37,000,000/- ambazo kati ya hizo Milioni 30,000,000/-
zimewagusa Wananchi wenyewe wa Kaya Maskini na zilizobakia milioni 7
zimepangwa kuhudumia wafanyakazi ambao wengine ni miongoni mwao.
zimepangwa kuhudumia wafanyakazi ambao wengine ni miongoni mwao.
Mapema Mkulima Maisuri Omar Suleiman kwa niaba ya wakulima wenzake wa
Bonde hilo la Kidau Ndagoni wameishukuru Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar kwa uamuzi wake wa kuwapatia mradi wa Tasaf ambao wameueleza
kuwa umeleta ukombozi mkubwa kwao.
Mkulima Maisuri alisema wakulima na wananchi wa Vijiji vilivyo
jitrani na Bonde hilo wamepata faraja kubwa kupitia Mfuko wa Tasaf
jambo ambalo kwa kiasi kuikubwa wamefanikiwa kupunguza ukali wa maisha
na kujiongezea kipato kinachoashiria kusaidia familia zao.
malengo yao waliyojipangia.
chanzo;zanzibar24.
Comments