Alisema
wakandarasi wazalendo, wameibuka kuwa na uwezo mkubwa wa kujenga majengo
yenye kuvutia na ya kudumu, ambayo yapo nchini na yanaendelea kutumiwa
na serikali.
Balozi Seif,
alitoa tamko hilo mara baada ya kufungua jengo la ghorofa mbili la
nyumba ya mkaazi kwa askari wa Uhamiaji na maofisa wake, eneo la Ndugu
kitu Chakechake Pemba, ikiwa ni sehemu ya shamra shamra za kutumia miaka
53 ya Mapinduzi Zanzibar yalioasisiwa mwaka 1964.
Alisema yapo
majengo ambayo yametumia gharama kubwa yaliojengwa na wakandarasi na
wasimamizi kutoka nje ya nchi na hatime mengine kabla ya kuhamiwa au
kukabidhiwa kwa serikali, yaliporomoko na kuitia hasara serikali.
Alisema jengo la
ZSSF lililopo Chakechake Pemba, limejengwa na mkandarasi mzalengo,
ingawa jengo la jirani yake lililojengwa na mkandarasi kutoka nje ya
nchi, lilianguka kabla ya ujenzi kukamilika.
Alieleza
wakanadarasi kutoka nje ya nchi, watalazimika kutumika tu pale ambapo,
kuna miradi mikubwa ambayo imeambata na ufadhili wake, na pengine
wakandarasi wazalendo hawana uwezo wa kuyajenga.
“Sisi serikalini
sasa tunasema kuwatumia wakandarasi wa nje bila ya sababu maalumu, na
iwe basi mbona hawa wazalendo wanajenga majengo madhubuti, si mnaona
hili la Uhamiaji hapa Ndugu kitu liko safi’’,alisema.
Katika hatua
nyengine Makamu huyo wa Pili wa Rais Zanzibar alisema, Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar na ile ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
zitaendelea kuwajengea wapiganaji wake makaazi bora kila hali ya fedha
itakaporuhusu.
Aidha aliwataka
wapiganaji hao wa Uhamiaji watakabahatika kukaa kwenye nyumba hiyo mpya
na ya kisasa, kuhakikisha wanaitunza ili iweze kudumu kwa muda mrefu.
Hata hivyo
ameitaka Idara hiyo ya Uhamiaji, kuhakikisha wanaifanyia matengenezo
nyumba hiyo, kila wakati utakapofika na sio kuiacha hadi kuharibika.
Mapema Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya ndani ya nchi, Meja Generali: Projestus
Rwegasira aliomba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, kuendelea
kuwapatia maeneo mengine kwa ajili ya kujenga nyumba za kuishi watendaji
wa Uhamiaji.
Mapema Kamishina
wa Uhamiaji Zanzibar, Johari Massoud Sururu, alisema Uhamiaji iliamua
kujenga nyumba hiyo ya ghorofa mbili, kwa ajili ya kupunguza tatizo la
makaazi kwa watendaji wake.
Nae Waziri katika
afisi ya Makamu wa Pili wa rais Zanzibar Mhe: Mohamed Aboud Mohamed,
alisema Idara ya Uhamiaji imefikia lengo la Mapinduzi matukufu ya
Zanzibar ya mwaka 1964 yenye azma ya kuwa na makaazi bora na ya kisasa.
“Lengo la
Mapinduzi ambayo leo tumo kwenye shamra shamra za kutimiza miaka 53,
yalikuwa ni kutukomboa na kisha kuhakikisha tunakuwa na makaazi bora na
imara”,alisema.
Mkuu wa Mkoa wa
kusini Pemba Mhe: Mwanajuma Majid Abdalla, alisema neema ya Mapinduzi ya
Zanzibar ya mwaka 1964, imeshasambaa kila kona ya mkoa wake, ikiwa ni
pamoja na huduma za afya, maji safia na salama na mawasiliano ya
barabara.
Jengo hilo la
ghorofa mbili, ambalo lilianza ujenzi wake mwezi Juni mwaka 2015, na
kukamilika Novemba mwaka jana, litakuwa na uwezo wa kukaliwa na familia
sita, na limetumia zaidi ya shilingi milioni 989, ambazo zimetolewa na
Idara ya Uhamiaji Zanzibar.
chanzo;zanzibar24.
Comments