Mkazi huyo Rashid Nassoro, baada ya kuwaua watu wake wa karibu
alikimbia na baadae kujaribu kujiua kwa kujichoma kisu tumboni na
kujaribu kukata sehemu zake za siri.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Khamis Selemani amethibitisha tukio
hilo na kusema lilitokea juzi eneo la Bukene, wilayani hapa baada ya
Rashid Nassoro (22) kumuua mkewe kwa kumchoma visu tumboni.
Alisema, baada ya kumuua mke wake, Rashid alimnyonga mtoto wake wa miezi minne na kukimbia.
Kamanda Selemani, alisema baada ya kukimbia Rashid aliamua kutaka
kujiua kwa kujichoma kisu tumboni na kujaribu kukata sehemu zake za
siri.
Alisema chanzo cha tukio hilo ni mwanamke kumtuhumu mume wake kuwa
ana uhusiano na mwanamke mwingine jambo lililomchukiza mwanaume huyo.
chanzo;habarileo.
Comments