
Kamanda wa Polisi
mkoani humo, Sheihan Mohamed Sheihan alisema baada ya kuona wanafamilia
wanashindwa kutoa ushirikiano, sasa Jeshi hilo linaangalia uwezekano wa
kuwatumia askari hao, ili kumtia mikononi mtuhumiwa huyo aliemuua kaka
yake Massoud Amour Seif.
Alisema Jeshi la
Polisi, linazo mbinu kadhaa za kumsaka mtuhumiwa na kama wanafamilia
wanashindwa kutoa ushirikiano, wao wataendelea kumtafuta kwa mbinu za
kitaalamu na wanazozijua wao.
Kamanda huyo
alisema kwa kuanzia tayari, wameshasambaza picha ya mtuhumiwa huyo
kwenye mitandao ya kijamii, ili kuonyesha kwamba bado anatafutwa na
vyombo vya ulinzi na usalama.
“Ijapokuwa
tulitarajia kuwa wanafamilia hao waliouliwa ndugu yao washirikiane na
sisi kumtafuta, lakini hawatowi ushirikiano sasa sisi Polisi,
tunazombinu za kumpata’’,alifafanua.
Hata hivyo
Kamanda huyo aliwataka wananchi wengine ambao wanamfahamu mtuhumiwa
huyo, wasisite kutoa taarifa kwa vyombo vya ulinzi na usalama, pale
watakaposikia tetesi za kuwepo.
Aidha amewaahidi
wananchi kuwa mtuhumiwa huyo hata kama amekimbilia nchi za Kenya, Uganda
au pengine popote, wasiwe na wasiwasi, jeshi hilo litamshika na kisha
kumfungulia mashitaka.
Katika hatua
nyengine, amesema tayari jalada la kesi yake lipo na linamsubiri
mtuhumiwa huyo, na atakapopatikana ili afunguliwe mashitaka, katika
vyombo vya kisheria kwa tuhuma zinazomkabili.
Disemba 1, mwaka
huu Kassim Amour Seif Abdalla mkaazi wa Mtambile wilaya ya Mkoani,
alivikimbia vyombo vya ulinzi na usalama, baada ya kudaiwa kumuua kaka
yake wa damu, nje ya kituo cha Polisi Mtambile, kwa ugomvi ulioanzia kwa
wake zao, ambapo hadi sasa hajapatikana.
chanzo;zanzibar24.
Comments