Akijibu swali katika Kikao cha Baraza la Wawakilishi huko Chukwani
Waziri wa Biashara ,Viwanda na Masoko Balozi Amina Salum Ali amesema
mbali na matatizo yanayoikabili Shirika la Viwango Zanzibar ZBS katika
kutekeleza wajibu wao ikiwemo uhaba wa maabara lakini bado wanaendelea
na ukaguzi wa bidhaa kupitia mfumo wa Pre export Verification of Xonformity .
Hata hivyo amesema mfumo huo umekua ukitumika Nchi nyingi ulimwenguni
ili kukuza maendeleo ya biashara pamoja na kusaidia kuondoa msongamano
wa mizigo bandarini.
Aidha amesema matumizi ya ukaguzi kupitia Mfumo wa Pre export Verfication of Xonformity
unarahisisha kupima bidhaa zinazotoka nje ya Nchi na zinazozalishwa
Nchini ili kutambua ubora wa bidhaa hizo na kuepuka kuleta athari kwa
matumizi ya Binaadamu.
Miongoni mwa bidhaa zinazofanyiwa ukaguzi ni pamoja na vyombo vya
moto aina ya magari yanayotoka nchi mbalimbali ikiwemo Japani,Singapoore
na Hongkong ambapo ukaguzi huo umeanza Agost1 mwaka huu .
chanzo;Zanzibar24.
Comments