Walioiba milioni 11 benki watiwa mbaroni.

Watu 12 wanashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani kigoma kwa tuhuma za kukutwa na kadi 100 za mashine za kutolea fedha(ATM) za mabenki tofauti tofauti.

Watu hao walikuwa wamekwishafanikiwa kutoa fedha katika mashine za kutolea fedha(ATM) kiasi cha shilingi milioni 11.

Kufuatia tukio hilo wananchi wametahadharishwa kuwa makini na wahalifu na matapeli na kwamba watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani mara baada ya uchunguzi kukamilika.

chanzo: zanzibar24.
 

Comments