Akizungumza katika maadhimisho ya siku ya ukimwi duniani mjini
Zanzibar amesema katika miaka ya hivi karibuni imeonekana kuongezeka kwa
tabia hatarishi ambazo zinaweza kuchangia kuongezeka kwa maambukizi
kutokana na jamii kuondokana na hofu ya kuambukizwa ugonjwa huo.
Kwa upande wake makamo mwenyekiti wa bodi ya tume ya ukimwi Zanzibar
Hasina Hamadi amesema madhimisho ya siku ya ukimwi hulenga zaidi
katika kuogeza uelewa juu ya changamoto zinazoikabili dunia katika
maambukizi ya virusi vya ukimwi.
Kwa mujibu wa takwimu wa mwaka 2013 zinaonesha asilimia 40 ya
wagonjwa wapya ni vijana wenye umri wa miaka kumi na tano hadi 24
kati yao asilimia 60 ni wanawake .
chanzo; zanzibar24.
Comments