Taarifa kutoka Ikulu: Rais Magufuli amtumia salamu za rambirambi kufutia kifo cha SACP Peter Kakamba.

Katika
salamu hizo Rais Magufuli amesema anaungana na askari wote wa Jeshi la
Polisi, familia ya marehemu, ndugu, jamaa na marafiki wote walioguswa na
kifo cha SACP Peter Kakamba katika kipindi hiki kigumu cha majonzi.
“Natambua
mchango mkubwa alioutoa Marehemu (SACP) Peter Kakamba katika Jeshi la
Polisi na katika jukumu kuu la ulinzi wa raia na mali zao, kwa hakika
tumempoteza kiongozi aliyekuwa akifanya kazi zake vizuri” amesema Rais Magufuli.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
chanzo;mpekuziblog.
Comments