Imesema ni marufuku shule kumkaririsha darasa, kumfukuza, kumhamishia
shule nyingine au kumsajili kama mtahiniwa binafsi (PC) mwanafunzi kwa
kigezo cha kutofanya vizuri katika mitihani ya shule husika.
Katibu Mkuu wa Chama cha Wamiliki wa Shule na Vyuo Binafsi
(Tamongosco), Benjamin Nkonye, alisema kuwa utaratibu wanaoutumia ni
kushauriana na wazazi wa wanafunzi wanaoshindwa kufanya vizuri shuleni
ikiwamo kuwapeleka katika vyuo vya ufundi (Veta).
chanzo: zanzibar24.
Comments