Sherehe za Maulid: Waziri Nchemba awataka Watanzania kuwafichua watu wanaotumia dini kufanya vurugu.
Waziri
wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Lameck Nchemba amewataka Watanzania wote
nchini kuungana kwa pamoja na kuwataja watu ambao wamekuwa wakifanya
vitendo vya vurugu kwa kuhusisha vitendo hivyo na dini kwani watu hao
wanaweza kusababisha nchi kupoteza amani.
Waziri
Nchemba ameyasema hayo katika sherehe za kitaifa za Maulid ambazo
zimefanyika mkoani Singida ambapo alisema mtu ambaye anamcha Mungu
hawezi kuwa akijihusisha na vitendo hivyo na Serikali ya awamu ya tano
itakuwa ikimchukulia hatua mhusika bila kuhusisha dini.
“Wizara
yangu inahusika na taasisi zote zinazohusika na ibada, niwambie jambo
moja tutofautishe udini na kumcha Mungu, mtu anaposhika sana dini ni
mshika dini na mtu unanayemcha Mungu ni mchaMungu sio mdini, makosa yote
katika nchi yanafanywa na makundi mawili ya watu wenye dini na wasio na
dini,
“Kosa
lolote ambalo likifanywa liwe kosa la ambae alifanya kosa, sio kosa la
dini, akifanya Mkristo kosa la mtu sio la dini, akifanya Mwislamu kosa
ni lake si la dini, na hata kama hana dini kosa ni lake yeye, na
tusaidiane kuwa tunawafichua wanaosababisha vurugu,” amesema Nchemba.
Pia
Nchemba ametumia nafasi hiyo kueleza kuwa amekabidhi msaada wa mabati
1,000 kwa ajili ya kutumika kujenga misikiti na kuahidi kuwa baada ya
wiki moja atawapatia gari aina ya Noah.
chanzo;mpekuziblog.
Comments