Wakichangia hoja binafsi kuhusu matokeo hatarishi katika sekta ya
uwekezaji wa Viwanda nchini iliyowasilishwa katika baraza la wawakilishi
zanzibar baadhi ya Wajumbe wa Baraza hilo wamesema ni aibu kubwa kwa
wananchi kufanya uharibifu wa makusudi kwa raslimali za wawekezaji na
kusababisha hasara kubwa.
Aidha wajumbe hao wametowa wito kwa muwekezaji wa kiwanda cha sukari
mahonda kuimarisha ulinzi wa kutosha katika mashamba yake pamoja na
kuweka mashamba katika hali ya usafi ili kujikinga na majanga ya moto
yanayojitokeza mara kwa mara.
Kwa mujibu wa tathmini iliyotolewa katika hoja hiyo binafsi
iliyowasilishwa barazani hapo na Mwakilishi wa Jimbo la Mpendae Mohammed
Saidi Dimwa amesema jumla ya Eka 902 zimeharibiwa katika matukio
tofauti ya uchomaji moto katika mashamba ya miwa ya Kiwanda cha Sukari
mahonda na kusababisha hasara ya zaidi ya shilling Bilioni 9 na million
mia saba kwa muwekezaji wa kiwanda hicho.
chanzo; zanzibar24.
Comments