Serikali ya Tanzania imesema inaendelea kuunga mkono serikali ya palestina.

palestinaSerikali ya Tanzania imesema inaendelea kuunga mkono serikali ya palestina juu ya maamuzi yaliyopitishwa na Umoja wa kimataifa  ya kupigania uhururu katika nchi yao.

Akizungumza na waandishi wa habari nnje ya Mkutano wa kimataifa wa kuunga mkono harakati za palestina Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rasi Muhammed Aboud Muhammed amesema wananchi wa Tanzania wanasikitishwa na matatizo yanayowakumba wapalestina juu ya kukosa haki zao za msingi ikiwemo kushindwa kuendelea na shughuli za kiuchumi.

Aidha ametowa wito kwa Nchi ya palestina na izrail kukaa pamoja katika kutafuta muafaka wa kumaiza migogoro iliopo ili waweze kunufaika na rasilimali zilizopo Nchini kwao.

Nae Balozi wa Palestina nchini Tanzania Alvaro Rodriguz amesema  anawashukuru watanzanikwa  kuunga mkono juhudi za kutafuta uhuru wa Nchi yao na kuahidi kuendelea kupambana katika kutafuta muafaka wa matizo yaliopo ili waweze kuimarisha maendeleo  na kuondoa udhalilishaji unaofanywa na Nchi ya Izrail.

img_2647Kwa upande wake Mkuu wa Chuo cha State Univarsity  of Zanzibar SUZA Prof. Idrisa Rai amesema mbali na wanafunzi wa Vyuo vikuu kupewa taaluma mbalimbali lakini pia walimu wa Vyuo vikuu wanajukumu la kufundisha mada maalumu ikiwemo historia ya palestina ili waweze kutoa elimu kwa wananchi juu ya vyanzo vya migogoro inayowakabili.

chanzo;zanzibar24.

Comments