MKURUGENZI wa Idara
ya Uvuvi Zanzibar Mussa Aboud Jumbe, Maofisa wa Uvuvi Kisiwani Pemba, kufanya
kazi kwa umoja , ili kwenda sambamba na malengo ya Serikali kufikia Uvuvi wa
kina kirefu cha maji.
Akizungumza na
maofisa wa Idara ya Uvuvi Pemba, huko katika ukumbi wa Wizara ya kilimo,
Maliasili, Mifugo na Uvuvi Weni Wete Pemba, amesema Serikali imeandaa mipango
imara ambayo itawawezesha wavuvi kuvua kwa kutumia vyombo vya kisasa.
Amesema Serikali kwa hatua nyengine
itastawisha Uvuvi mdogo mdogo , ili uweze kufikia Uvuvi wa kina kirefu jambo
ambalo litasaidia maisha ya wavuvi.
Nae Mkuu wa Idara ya
Uvuvi Pemba, Sharif Mohammed Faki, Amesema Serikali inaendelea kutoa mafunzo
kwa vijana, ili wapate taaluma ambayo itawawezesha kufanikisha azma
iliyokusudiwa ya kufikia uvuvi wa bahari kuu.
Aidha amesema kuwa,
suala la Uvuvi haramu linaendelea kupigwa vita kwa kufanya doria pamoja na
kushirikiana na kamati za shehia kwa kupeana taarifa kila linapotokea tatizo.
Sambamba na hayo
amesema kuwa, katika utekelezaji wa shughuli hizo pia kutakua na kampuni maalum
itakayosimamia kwa kutoa vitendea kazi , ili kufikia malengo yaliokusudiwa.
Comments