Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi: Zanzibar inakabiliwa na tatizo kubwa la ukatili wa kijinsia linalotokana na upungufu wa sheria.
Akifungua kongamano la wanaharakati wa Kupinga ukatili na
Udhalilishaji wa Kijinsi Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi Mgeni
Hassan Juma amesema Zanzibar bado inakabiliwa na tatizo kubwa la ukatili
wa kijinsia linalotokana na upungufu wa sheria.
Hata hivyo amesema pindipo sheria zilizopo zitarekebishwa na kufuatwa
itasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza kasi ya uwepo wa vitendo vya
ukatili wa kijinsia vinavyowarejesha nyuma kimaendeleo watu wanaofanyiwa
vitendo hivyo.
Kwa upande wao washiriki wa kongamano hilo wametowa wito kwa serikali
kuanzishwe mahkama ya Udhalilishaji pamoja na kutolewa sheria kwa
lugha ya Kiswahili ili ziweze kurahisisha wakati wa kutafuta suluhu ya
matukio ya Udhalilishaji wanapofika mahakamani.
Akiwasilisha mada ya juu ya hali halisi ya ukatili wa kijinsia
Zanzibar Juma Omar Abdallah amesema mbali na taasisi za harakati za
kijinsia kuwa mstari wa mbele katika kutatua matatizo yanayojitokeza
katika jamiii lakini bado wanarejeshwa nyuma na hukumu ndogo
wanazopatiwa watuhumiwa jambo ambalo linachangia kuengezeka kwa vitendo
hivyo Nchini.
chanzo; Zanzibar24.
Comments