MZEE Athuman Mchambua (76), ambaye ameweka tangazo nyumbani kwake la kutafuta mke, ameongeza sharti jipya kwa mke anayemuhitaji.
Amesema
licha ya kupokea simu nyingi kutoka maeneo mbalimbali nchini, lakini
amewataka wanawake ambao atawafanyia usaili, hasa kwa yule ambaye
atakuwa ameshinda, kutobweteka kwani atakuwa katika kipindi cha mpito
cha ndoa yake.
Mzee
huyo amelieleza gazeti la Mtanzania kuwa amefikia hatua hiyo ili
kuanza kupitia majina ya wanawake zaidi ya 30 ambao tayari wamejaribu
bahati ya kuolewa naye.
Alisema
kuwa haoni haja tena ya kuendelea kuweka tangazo hilo kwa kuwa asilimia
kubwa ya wanawake wanaojitokeza hushindwa kukidhi vigezo
anavyovihitaji.
Alivitaja vigezo sita muhimu vya mwanamke anayemuhitaji kuwa ni awe mcha Mungu na mwenye kutunza watoto wake.
“Vigezo
vingine awe na sifa ya ndoa, awe na sifa ya mume, awe na sifa ya
kilimo, awe na sifa ya kutunza watoto na awe na sifa ya usafi wa hali ya
juu.
“Tangu
kuanza nimepata wanawake zaidi ya 30 ambao wanne kati yao wamefika hapa
nyumbani kwangu, lakini wengine wamekuwa wakiona aibu kuja hapa moja
kwa moja na hivyo wamekuwa wakitumia simu. Leo (jana) nimewafanyia
usaili wanawake watano kwa simu, lakini hakuna hata aliyefuzu nusu ya
vigezo, wengi wamekuwa wakiteleza sifa ya kilimo,” alisema.
chanzo;mpekuziblog.
Comments