MHAGAMA ATAKA JPM APEWE MUDA ILI ATEKELEZE AHADI ZAKE.

Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu, Jenista Mhagama amewataka wafanyakazi nchini kumpa muda Rais John Magufuli wa kushughulikia changamoto zao pamoja na ahadi alizowaahidi katika maadhimisho ya siku ya wafanyakazi yaliyofanyika Mei Mosi, 2016.
Mhagama alitoa wito huo Desemba 19, 2016 wakati akizungumza na Kamati ya Wanawake Taifa ya Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi nchini (TUCTA) baada ya Katibu wa Shirikisho hilo Yahya Msigwe kumuomba amkumbushe Rais Magufuli juu ya utekelezwaji wa ahadi hizo.
Baadhi ya ahadi alizozitoa Rais Magufuli siku hiyo, ni pamoja na kupunguza makato ya mishahara hasa kwa wanaolipwa mishahara ya kima chini na ongezeko la mishahara na masilahi kwa wafanyakazi wanaopandishwa daraja.
“Siku ya wafanyakazi rais alijipambanua kutetea masilahi wafanyakazi pamoja na kutoa ahadi, mumpe nafasi ili ahakikishe changamoto za wafanyakazi zinatatuliwa,” amesema na kuongeza.
“Serikali itaendelea kufanya kazi na TUCTA , na navishauri vyama vya wafanyakazi visiwe na makundi bali viungane kubainisha changamoto za wafanyakazi ili zifanyiwe kazi.”
Aidha, ameagiza kamati ya wanawake kuandaa mkakati utakaosaidia kuondoa changamoto ya ukatili wa kijinsia hasa kwa wanawake.
Pamoja na kuhakikisha waajiriwa wote nchini wanazijua sheria za kazi ili kuepukana na migogoro mbalimbali inayohusu ajira.
chanzo;zanzibar24.

Comments