Siku
moja baada ya mfanyabiashara Yusuf Manji kuhama kwenye jengo la Quality
Plaza, uongozi wa kampuni ya udalali ya Yono umesema kinachosubiriwa ni
mfanyabiashara huyo kulipa deni au kukamatwa kwa mali zake.
Akizungumza
jana, Mwenyekiti wa Bodi ya kampuni hiyo, Stanley Kevela alisema Manji
alipewa siku 14 zilizoanza kuhesabiwa tangu Jumamosi ili kulipa deni.
Alisema
endapo siku hizo zitamalizika bila kulipwa, mali za mfanyabiashara huyo
zitakamatwa ili kufidia deni la Dola 6.1 milioni za Marekani (zaidi ya
Sh13 bilioni) anazodaiwa.
Kevela
alisema fedha hizo ni gharama ya kupanga kwenye jengo hilo ambalo ni
mali ya Mfuko wa Pensheni wa Watumishi wa Umma (PSPF).
Alisema baada ya kukamilika kwa mchakato huo, kampuni italikabidhi jengo hilo kwa PSPF kwa ajili ya shughuli nyingine.
Mfanyabiashara huyo alipotafutwa jana ili kuzungumzia suala hilo, simu yake ya mkononi haikupatikana.
Mkurugenzi wa kampuni ya Yono, Skolastika Kevela alisema kazi ya kuondoa mali za mpangaji kwenye jengo hilo ilikamilika juzi.
“Kampuni
zote zimeshaondoa vifaa na milango ya jengo hilo imefungwa kwa kufuli
za kampuni yetu. Tutalisimamia jengo hadi tutakapowakabidhi PSPF,” alisema.
Uamuzi
wa Manji kuhamishwa kwenye jengo hilo ulitolewa na Mahakama kutokana na
kushindwa kulipa kodi ya pango ambapo alipewa masaa 24 ya kuondoa
vitu vyake.
chanzo;mpekuziblog.
Comments