MAKAMU
wa Rais, Samia Suluhu Hassan amewataka wazazi na walezi wa visiwani
Zanzibar, kuacha tabia ya kuwaoza wasichana wakiwa na umri mdogo, bali
wawasomeshe kwa ajili ya manufaa yao ya jamii kwa ujumla.
Samia alisema hayo kwa nyakati tofauti, wakati akizindua madarasa ya kisasa iliyojengwa kwenye eneo la Kilimani na kukagua ujenzi wa vyumba vya madarasa na ujenzi wa msikiti mkubwa kuliko yote nchini Tanzania unaojengwa katika eneo la Ijitimai Kidoti mkoani Kaskazini Unguja.
Ujenzi huo unafanywa kwa michango ya wananchi. Alisema hayo katika siku yake ya kwanza ya ziara ya Kikazi Unguja.
Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Makamu wa Rais, Zanzibar, ilieleza kuwa makamu huyo wa Rais yupo katika ziara visiwani Zanzibar.
Kwa
mujibu wa taarifa hiyo, Samia alisema kama wazazi na walezi watasomesha
watoto wa kike, elimu watakayopata itasaidia kwa kiasi kikubwa
wasichana hao, kufanya maamuzi sahihi na yenye tija katika jamii.


chanzo;mpekuziblog.
Comments