Mara baada ya kukamilisha shughuli ya uchunguzi wa afya yake Balozi Seif anatarajiwa kufanya ziara ya Kiserikali ya Siku Nne Nchini China atakayofuatana na Mkewe Mama Asha Suleiman Iddi, Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar Dr. Khalid Salum Mohamed na Naibu Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji Mh. Mohamed Ahmed Salum.
Wengine atakaofuatana nao ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Nd. Khamis Mussa Omar, Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora Nd. Asha Ali Abdulla.
Akiwa Nchini Jamuhuri ya Watu wa China Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar atapata fursa ya kutembelea Benki ya Kimataifa ya Exim na kufanya mazungumzo na Uongozi wa juu wa Benki hiyo yenye mafungamano na Zanzibar hasa katika Miradi mbali mbali ya Kimaendeleo.
Pia katika ziara hiyo Balozi Seif atatembelea Makamo Makuu ya Kampuni ya Kimataifa ya Mitandao ya kisasa ya Mawasiliano ya ZTE na kufanya mazungumzo na Uongozi wa Kampuni hiyo inayosimamia Mradi wa Mawasialiano Serikalini { E. Government }.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar na Ujumbe aliofuatana nao atamalizia ziara yake ya Kiserikali Dubai ambapo atapata fursa ya kufanya mazungumzo na Uongozi wa Wizara ya Biashara pamoja na kukutana na baadhi ya Viongozi wa Makampuni na Taasisi za Kibiashara watakaoonyesha nia ya kutaka kufungua milango ya Uwekezaji Miradi yao ya Kiuchumi na Biashara Visiwani Zanzibar.
chanzo;zanzibar24.
Comments