Mahkama chukueni jitihada kumaliza kesi za ukatili wa kijinsia.

Jeshi la polisi limetakiwa kutozifumbia macho kesi za ukatili wa kijinsia thidi ya wanawake na watoto ambazo zimeonekana kushamiri siku hadi siku.

Wito huo umetolewa na Naibu Waziri Wizara ya Afya Zanzibar Mh. HARUSI SAIDI SULEIMAN katika maadhimisho ya siku kumina sita za kunginda ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto  yaliofanyika katika Viwanja vya Jamhuri Wete Kisiwani Pemba.

Amesema  jamiii  inashindwa kupeleka kesi hizo mahakani  kutoka na kuchelewesha kwa baadhi ya kesi na kuchukua muda mrefu jamba ambalo linavunja moyo kwa walio pata matatizo kama hayo .

Amefahamisha kua  Jeshi la Polisi kuzichelewesha kesi hizo nakuzipeleka mahala husika  kuna pelekea jamii kuzisuluhisha baadhi ya kesi kifamilia hali inayo ongeza kasi ya matendo ya ukatili wa  kijinsia  kuongezeka kwa kasi watendaji wakuu wakionekana kua niwatu wa karibu.

Aidha amesema ukosefu wa malezi ya pamoja umechangia  kuongezeka kwa vitendo vya ukatili wa kijisia na kwamba awali vitendo hivyo vilikuwa vimepungua kwa kuwepo mashirikiano katika jamii.

Hatahivyo ameliomba jeshi la Polisi na jamii kwa ujumla  kushirikiana kwa pamoja ili kutokomeza vitendo hivyo ambavyo kwa sasa vimeonekana kushika kwasi wa vija wa kiume.

Kwaupande wake Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba OMAR KHAMIS OTHMAN kupitia maadhimisho hayo amepiga marufuku uoneshwaji wa televishe nje ndani ya mkoa huo  nakudai kua kitendo hicho kimechangia kwa aslimia kubwa vijana na watoto kujiingiza katika vitendo viovu.

Amelitaka  jeshi la polisi kuwa chukulia hatua za kisheria wale wote watakao bainika kuonyesha televishen nje na adhabu kali zitolewe juu yao kwa kupinga amri hiyo.

Kamanda wa POLISI Mkoa Wa Kaskazini Pemba HAJI KHAMIS HAJI amesema kuundwa kwa madawati ya kupinga ukatili wa kijinsia kunaweza kupunguza vitendo hivyo kutoendelea pindi jamii itakapo shirikiana na makundi hayo na kutoa ushahidi pale wanapo hitajika ili iwe rahisi kuwachukulia hatua walio husika na ukatili huo.

Awal  akisoma risala katika maadhimisho hayo  WP11892P/C REHEMA  kutoka mtandao wa Polisi wanawake mkoa wa Kaskazini Pemba amesema ukosefu  wa kipimo cha DNA na ofisi za madawati ni miongomi mwa channgamoto zinazo wakabili katika utendaji wao wakazi.

Amesema ucheleweshwaji wa kutolewa maamuzi kwa  kesi zianazopelekwa mahakamani  kuna sababisha baadhi ya watu kukata tamaa  juu ya kesi wanazo ziwasilisha na mwisho kukosa mashahidi waliojitolea kutoa ushahidi juu ya vitendo husika.

Ameeleza kua jamii imekosa ujasiri juu ya kuwakamata wahalifu wanaofanya matendo hayo ikiwemo unyanyasaji mkubwa wa liwati ambalo linashika kasi kwa jamii.

Ametanabahisha  kuwa  jumla  ya  kesi 74 zimeripotiwa kwa mwaka 2016 ambapo kesi16 mashauri yake yanaskilizwa kesi 24 zimetolewa hukumu kwa watuhumiwa kutumikia kifungo, kesi 3 zipo kwa mkamia mkuu wa serekali na kesi 26 zinaendelea na upelelezi.

 Madawati ya mtandao wa polisi wanawake yalianzishwa mwaka 2007 na aliekua kamishna mkuu wa jeshi hilo SAID ALI MWEMA kwa lengo la kupambana na vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia kwa wanawake na watoto .

Ujumbe wa mwaka huu katika maadhimisho hayo ni FUNGUKA PINGA UKATILI WA KIJINSIA TOA ELIMU SALAMA KWA WOTE.

Comments