Akizungumza na waandishi wa habari hizi, huko ofisisni kwake chake chake,mdhamana wa ofisi ya mkurugenzi wa mashtaka Pemba, Ali Rajab Ali amesema jumla kya kesi hizo zimefutwa kufuatia maahakama kutoridhika na ushahidi pamoja na kile kiunachodaiwa kuwa ni kumalizana nje baina ya wenye kesi kala kufika kurejea mahakani.
Amesema, katika kipindi cha wiki moja iliyopita alipokea jumla ya kesi 5 ambapo kesi 4 zilikuwa ni za ubakaji na udhalilishaji na kesi 1 na wizilakini mwisho kesi hizo huwa zinamalizika kiajabu .
Alisema kesi za ubakaji na udhalilishaji huwa zinawapa changamotokatika uendeshaji wake hususan upande awa mashahidi.
” kwa upande wa mashahidi huwa tunapata shida sana hususan kwa watoto walio chini ya umri wa miaka 7 ambao mara nyingi huwa hata kusema hawawezi”
Hivyo aliwaomba wananchi kuwa na utamadunoia wa kutoa ushahidi pale amabpo unahitajika ili kuokomesha kabisa matendo ya udhalilishaji ambayo yanashamiri siku hadi siku.
chanzo;zanzibar24.
Comments