JAJI Mkuu wa Tanzania, Mohammed Chande Othman, amewaasa mawakili kuacha tabia ya kutumwa vibaya na wateja wao kwa kuchelewesha kesi mahakamani, kitu ambacho ni kinyume na maadili ya kazi hiyo.
Aidha, Jaji Chande amesema pia kuwa mbali na mawakili, pia Polisi, ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na mahakama, nao wanachangia mrundikano wa kesi, hivyo kukwamisha masuala mbalimbali.
Amezitaka taasisi hizo, kutotumika kuchelewesha kesi, badala yake waisaidie mahakama katika mpango mkakati wake wa kupunguza mrundikano wa kesi.
Alisema hayo wakati wa hafla ya kuwaapisha mawakili wapya 285, iliyofanyika Viwanja vya Karimjee, Dar es Salaam jana. Kuapishwa kwao kunafanya idadi ya mawakili nchini kufikia 6,082. Jaji Othman alisema kuwa wapo baadhi ya mawakili, wanatumiwa na wateja wao kwa ajili ya kuchelewesha kesi, kitu ambacho ni kinyume na maadili ya kazi hiyo.
“Tunawasisitiza mawakili hawa wawe sehemu yaLipumba mrundikano wa kesi ili kufikia mipango mikakati yetu ya miaka mitano kuanzia 2015 hadi 2020,” alisema Chande.
Aidha, alisema kuwa wamepokea asilimia 71 ya malalamiko kutoka kwa wananchi, ambapo asilimia 45 ya malalamiko hayo, yalionekana kuwa ya kweli kwamba wanasheria wafanya kazi zao bila kuzingatia taratibu na maadili yaliyowekwa.
chanzo;zanzibar24.
Comments