Katika salamu hizo za rambi rambi, Dk. Shein alieleza kuwa amepokea kwa huzuni kubwa taarifa ya kifo cha Bregedia Jenerali Cyril Ivor Mhaiki, Kamanda wa Brigedia ya Nyuki Zanzibar, kilichotokea jana katika Hospitali ya Jeshi la Wananachi wa Tanzania, Lugagalo, Dar-es-Salaam.
Dk. Shein kwa niaba yake binafsi pamoja na wananchi wote wa Zanzibar, alieleza kuwa wamepokea kwa mshtuko, taarifa ya kifo cha Kamanda huyo hodari aliyetoa mchango mkubwa katika shughuli za ulinzi na usalama na maendeleo ya nchi.
“Siku zote, Kamanda Mhaiki alikuwa mtu mwenye mashirikiano na wenziwe, muadilifu, msikivu na mahiri katika kazi zake”ilisema sehemu ya salamu hizo za rambi rambi.
Aidha, salamu hizo za rambirambi zilieleza kuwa hakika Marehemu Mhaiki ameacha pengo kubwa kwa familia yake, Brigedi ya Nyuki, Jeshi la Wananachi wa Tanzania pamoja na nchi nzima kwa jumla huku akisisitiza kuwa mchango wake hautosahaulika.
Dk. Shein alimuomba Jenerali Mwamunyange kuzifikisha salamu hizo za rambirambi kwa Wanafamilia, Maofisa na Wapiganaji wa vikosi vyote vya Ulinzi na Usalama.
chanzo; Zanzibar24
Comments