Kauli hiyo imetolewa na Makamu wa Rais wa Benki hiyo Bwana Sun Ping
wakati wa mazungumzo yake na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi
Seif Ali Iddi anayeuongoza Ujumbe wa Viongozi Wanne wa Serikali
akimalizia ziara yake ya Kiserikali ya Siku Tano Nchini China.
Bwana Sun Ping alisema Taasisi hiyo ya Fedha ya China imeridhika na
hatua kubwa ya maendeleo iliyofikiwa na Zanzibar katika kuimarisha
uchumi wake kiasi kwamba Benki hiyo itaangalia namna za kusaidia nguvu
katika kuona miradi inayoanzishwa inatekelezwa.
Makamu wa Rais wa Benki hiyo ya Exim alimueleza Balozi Seif na Ujumbe
wake kwamba Tanzania ndio nchi pekee iliyopewa kipaumbele na benki
hiyo katika kupatiwa mikopo na misaada ikilinganishwa na Nchi nyengine
Barani Afrika.
Akitoa shukrani zake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif
Ali Iddi aliipongeza Benki hiyo ya Exim kwa ukarimu wake wa kuunga mkono
miradi ya Maendeleo inatotekelezwa na Zanzibar kwa njia ya misaada na
hata mikopo.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
23/11/2016.
chanzo: zanzibar24.
Comments