Balozi Seif atoa wito kwa wenye Vilabu vya Pombe kufuata Sheria.

baraza-la-wawakilishiMakamo wa Pili wa Rasi Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amesema  wamiliki wa Baa na Vilabu vya Pombe wanawajibu wa kufanya  kazi kwa kufuata sheria walizopewa ikiwemo kuepuka kujenga baa zao katika makaazi ya wananchi ili kulinda mila na desturi za mzanzibari.

Akihutubia  Baraza la wawakilishi kabla ya Kuhairishwa kwa Baraza hilo huko Chukwani Balozi seif  amesema kumekuwa na malalamiko mengi kutoka kwa wananchi juu ya uwepo wa  vilabu na baa usiozingatia taratibu za sheria.

Hata hivyo ametoa wito kwa wamiliki wa vilabu vya Pombe na mabaa kuwa na utaratibu maalumu wa kupiga miziki ili kuepuka kuwakera wanakijiji hususani katika wakati wa usiku.

Akizungumiza suala la uvunjifu wa amani amesema kila mwananchi anajukumu la kulinda amani iliopo Nchi na kujiepusha kufanya mambo yanayoashiria kuvunja amani jambo ambalo linatapelekea  kuharibu maendeleo yaliopo.

Kikao cha Baraza la wawakilishi Zanzibar kimeahirishwa hadi ifikapo februari 15, 2017 ambapo jumla ya miswada minne imejadiliwa na Kupitishwa huku mswali 85 na maswali ya nyongeza 201 yameulizwa na kujibiwa katika baraza hilo .

chanzo; Zanzibar24.

Comments