Utiaji saini huo wa Kitabu cha Maombolezo ameufanya katika Makaazi ya
Balozi wa Jamuhuri ya Watu wa Cuba Nchini Tanzania uliopo Bara bara ya
Ali Bin Said Mtaa wa Namanga Jijini Dar es salaam.
Balozi Seif ameiwakilisha Serikali ya Mainduzi ya Zanzibar katika
utiaji saini huo akiambatana na Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Mh. Harus
Said Suleiman , Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar Mh. Mihayo Juma Nhunga pamoja na Mratibu Mkuu wa Ofisi ya
Uratibu wa shughuli za SMZ Dar es salaam Nd. Issa Mlingoti Ali.
Akimfariji Balozi wa Jamuhuri ya Watu wa Cuba Bwana Jorge Luis Loez
baada ya saini hiyo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali
Iddi alisema Kifo cha Jemedari huyo wa Taifa la Cuba hakikuacha pengo
kwa nchi hiyo lakini pia kimeigusa Tanzania kutokana na Mataifa hayo
kufanana katika harakati zao za kupigania Uhuru kutoka makucha ya
Kikoloni.
Balozi Seif alisema Jamuhuri ya Cuba ni kaka wa Tanzania katika njia
ya kusaidia maendeleo na nyanja za uchumi zilizopata ufanisi mkubwa
kutokana na kazi kubwa iliyofanywa na Wataalamu wa Nchi hiyo kuwawezesha
Kitaaluma wananchi Wazalendo wa Tanzania.
Akitoa shukrani zake Balozi wa Jamuhuri ya Watu wa Cuba Nchini
Tanzania Bwana Jorge Luis Lopez alisema Cuba itaendele kuwa mshirika
mkubwa wa Tanzania katika azma yake ya kuona wananchi waliowengi wa
ngazi ya chini wa Mataifa hayo wanafaidika na Uhuru walioupata kutoka
katika makucha ya wakoloni.
Balozi Lopez alisema Cuba na Tanzania zimeshirikiana kwa muda mrefu
uliobakia kuwa Historia kwa sasa hasa katika sekta za Afya, Kilimo,
Viwanda na masomo ya Elimu ya Juu, ushirikiano uliowekwa msingi wake na
Waasisi wa Nchi hizo Mbili Marehemu Mwalimu Julius K. Nyerere na Bwana
Fidel Castro.
Marehemu Fidel Castro alizaliwa Mnamo Tarehe 13 Agosti mwaka 1926
ndani ya familia ya watoto Sita akiwa watatu wa Mzee Angel aliyekuwa
mfanyakazi wa mashamba ya miwa akiwa na asili ya Taifa la Hispania.
chanzo; zanzibar24.
Comments