Tukio hilo la kumkamata kijana huyo limetokea majira ya saa nne Leo Asubuhi huko katika manispaa ya mji wa Zanzibar wakati mtuhumiwa huyo akijaribu kukimbia.
Baadhi ya wananchi walioshuhudia tukio hilo wamelimelipongeza jeshi la Polisi kwa kuweza kumdhibiti mtuhumiwa huyo alietenda kesi ya udhalilishaji.
Akizungumza na Zanzibar24 kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Mjini MagharIb Hassani Nassir amesema kuwa mtuhumiwa Omar Said Omar mwenye umri wa miaka 24 amekamatwa baada ya mtego wa jeshi la polisi kwa shambulio la hatari linalo mkabili.
Pia kamanda amesema kuwa mtu moja amekutwa amefariki katika maeneo ya bububu kihinani akiwa na majeraha mwilini na kuhifadhiwa katika hospitali ya mnazi moja uchunguzi wa polisi ukiendelea.
chanzo;Zanzibar24
Comments