Akizungumza na wandishi wa habari katika kuadhimisha siku ya ugonjwa
wa kisukari duniani waziri wa wizara hiyo Mh. Mahamoud Thabit Kombo
amesema ugonjwa huo umegunduliwa zaidi kwa watoto kutoka familia
masikini.
Amesema utafiti uliofanywa na wizara hiyo kuanzia mwaka 2010 hadi
2015 umegundua zaidi ya watoto mia mbili na ishirini (220) wenye umri
chini ya miaka mitano wanaugua ugonjwa wa kisukari kati yao 20
wamefariki dunia.
Aidha wizara hiyo pia imegundua zaidi ya wafanyakazi wa serikali 190
kati ya 600 waliochunguzwa afya zao hivi karibuni wamo katika hatari ya
kukumbwa na ugonjwa wa kisukari.
Waziri Kombo amesema takwimu hizo zinaonesha bado wananchi wanapuza
taaluma inayotolewa na watalaamu wa afya ya kujikinga na ugonjwa huo kwa
kutumia vyakula vya mafuta, kushindwa kufanya mazowezi na kupima afya
zao.
Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa Zanzibar mwaka 2011 umegundua zaidi
ya watu elfu 50 wanaugua ugonjwa wa kisukari wenye umri kati ya miaka 25
hadi 64.
Siku ya kisukari duniani huadhimishwa kila ifikapo Novemba 14 ya kila
mwaka na kwa hapa Zanzibar siku hiyo imeadhimishwa kwa makongamano na
mchezo wa mpira wa miguu.
chanzo;Zanzibar24
Comments