Wananchi walia na bei mpya ya umeme.

zeco
Watumiaji wa huduma za umeme majumbani wamelalamikia shirika la umeme Zanzibar ZECO kwa kuongezwa  bei ya nishati hiyo.

Wakizungumza na Zanzibar24 mara baada ya ZECO kuongeza bei ya umeme kwa asilimia 20 wamesema gharama za umeme bado ziko  juu kwa wananchi masikini hivyo wameiomba serikali kuingilia kati juu ya upandaji wa bei hizo.
Aidha wananchi wangine wameshauri serikali kuangalia njia mbada ya kutumia umeme wa jua au upepo usiokuwa na gharma kubwa za uzalishaji..
Shirika la umeme Zanzibar limepandisha bei ya umeme kwa asilimia 20 ambapo mtumiaji wa majumbani asiezidi uniti 50 kwa mwezi atalipia shilingi 79 kwa unit moja badala ya shilingi 66 za awali.
chanzo;zanzibar24

Comments