Wito huyo umetolewa na afisa kitengo cha elimu mjumwisho na stadi za
maisha Pemba Khamis Haji Hamadi wakati akitowa mafunzo ya siku moja kwa
walimu na wanafunzi juu ya athari za ndoa za utoto katika ukumbi wa
shule ya Madungu sekondari chake chake Pemba.
Amesema wameanda mafunzo hayo maalum baada yatafiti zilizofanywa na
jumuiya ya maimamu zanzibar na kugunduwa kuwa bado vitendo vya liwati na
ndowa za utotoni vinazidi kushamiri nchini.
Akitowa mafunzo juu ya athari ya mimba za utotoni afisa kitengo cha
cha elimu mjumwisho na stadi za maisha zanzibar amewataka wanafunzi
kuwacha kutumia utandawazi vibaya kwa mambo yasiokua na tija kwao na
badala yake kutumia kwaajili ya masomo na sivyenginevyo.
Nae mmoja wa wanafuni walioshiriki katika mafunzo hayo, Zainabu
Habibu Ali kutoka shule ya shamiani sekondari ameiomba wizara ya elimu
kuendeleza kutoa elimu siku hadi siku kwani kufanya hivyo kunaweza
kusaidia kupunguza vitendo hivyo vichafu, ambavyo vinadumaza maendeleo
ya watoto na wanafunzi.
Jumla ya wanafunzi 50 kutoka shule mbali mbali kisiwani pemba
wamepatiwa mafunzo hayo ikiwa lengo pia ni kuleta uelewa na mwanko kwa
wanafunzi hao hatimae kutojiingiza katika vitendo hivyo vichafu.
Chanzo; zanzibar24.
Comments