Wakulima wa mwani Zanzibar kutafutiwa faraja.

wakulima-wa-mwani-zbarWizara ya Kilimo ,Mali asili,Mifugo na Uvuvi Zanzibar imesema inaendelea na hatua ya kulipatia ufumbuzi tatizo la Bei ya zao la Mwani ili liweze kunufaisha wakulima wa zao hilo.

Akijibu swali kwa Niaba ya Waziri wa wizara hiyo katika kikao cha baraza la Wawakilishi huko Chukwani Naibu Waziri wa Kilimo ,Mali asili,Mifugo na Uvuvi Zanzibar Lulu Msham Abdallah amesema mbali na elimu ya Uhamasishaji wa kilimo cha zao hilo kutolewa kwa wananchi pia serikali inaendelea na juhudi za kutafuta wawekezaji watakao weza kusarifu mwani unaozalishwa.

Hata hivyo amesema kutokana na zao la mwani kuwa na Thamani kubwa katika soko la Dunia serikali imeandaa mkakati maalumu wa kuwahamasisha wawekezaji kuanzisha viwanda vya vya kusindika mwani ili kuimarisha bei ya zao hilo sambamba na kuengeza nafasi za ajira kwa Wananchi.

Aidha amefahamisha kuwa serikali imeandaa Kamati maalumu ilioshirikisha Wizara na Shirika la biashara Zanzibar ili kuongeza ushawishi katika zao la mwani kuuzwa na kunuliwa kama zao la karafuu.

Zanzibar ni sehemu ya tatu kwa udhalishaji wa zao la mwani ambapo lina wakulima wapatao 23 elfu na mia tano kati yao wengi ni wanawake.

chanzo; zanzibar24.

Comments