Wakulima wa mwani waaswa kuendelea na uzalishaji licha ya changamoto ya bei.

Wakulima wa Mwani Z’barWakulima wa mwani wilaya ya micheweni wametakiwa kuendelea kuzalisha zao hilo licha ya changamoto ya bei kutoka kwa makampuni yanayonunua zao hilo.
Wito huo umetolewa na katibu tawala wilaya hiyo Hamad Omar Small wakati akizungumza na wandishi wa habari ofisini kwake jana .

Amesema serikali inatambua bei ndogo ya zao na kwamba itaendelea kuyashaiwishi makampuni yanayonunua zao hilo ili kuweza kuongeza bei ya mwani .

Aidha small amewapongeza akinamama wa wilaya hiyo kutokana na juhudi walizianzisha za kujikomboa na umaskini kwa kuwapatia taaluma zaidi .

Licha ya kua zanzibar ni nchi ya tatu duniani inayasafirisha kwa wingi sokoni zao hilo ikitanguliwa na uphilipino na indonesia lakini bado wazalishaji wa zao hilo karibia wote wamekua wakilalamikia bei duni ya uuzaji wake tofauti na ugumu katika uzalishaji wake, ambapo wanasema hali hiyo huwakwaza na kuvunjika moyo katika uzalishaji wa zao hilo.

Bei ya zao hilo kwa kilo ni baina ya shilingi 600 na 700 na imewahi kushuka hadi kufikia shilingi 300.

chanzo; zanzibar24.

Comments