Akizungumza na mtandao huu, Wakati wa ziara ya ukaguzi wa bidhaa za vyakula na Vileo katika maghala mbalimbali Afisa wa Afya Manispaa ya Magharibi B Iddi Mbaraka amesema kuna baadhi ya wafanyabiasha wamekuwa wakiweka bidhaa kwenye maghala kwa muda mrefu hatimae kupita muda na kuuza kwa wananchi kwa bei nafuu jambo linalohatarisha maisha ya walaji.
Iddi amesema, katika ziara yao ya ukaguzi wamebaini bidhaa mbalimbali za vyakula zilizopita muda wake kwenye maghala na kusema kuwa hatua za kisheria zitachukuliwa na kuwazibiti wahusika wanaofanya ubabaishaji huo.
Aidha amesema hivi sasa udanganyifu umekuwa mwingi kwani hivi karibuni walikamata mafuta yaliyopita muda wake na kuyaangamiza ili kulinda watumiaji waliowengi.
chanzo;zanzibar24.
Comments