Shein aapisha manaibu waziri.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohamed Shein amewaapisha manaibu waziri wapya aliowateua hivi karibuni kushika nyadhifa katika wizara mbalimbali za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ).

Walioapishwa ni Mihayo Juma Nhunga, Mwakilishi wa Jimbo la Mwera ambaye anakuwa Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Shamata Shaame Khamis, Mwakilishi wa Jimbo la Micheweni anayekuwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalumu za SMZ na Shadya Mohammed Suleiman ambaye ni Mwakilishi wa Viti Maalumu kutoka mkoa wa Kaskazini Pemba kuwa Naibu Waziri wa Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Vijana, Wanawake na Watoto.

Mabadiliko madogo yaliyofanywa na Rais Shein katika Baraza la Mawaziri yamegusa manaibu waziri tu ambapo idadi yao imeongezwa kutoka wanne hadi kufikia saba.

Hafla ya kuwaapisha viongozi hao ilifanyika Ikulu mjini Zanzibar na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
chanzo;habarileo.

Comments