Serikali yasisitiza watoto kupatiwa haki zao za msingi.

barazaWizara ya Uwezeshaji,Wazee,Vijana wanawake na Watoto Zanzibar imesema inaendelea na Mpango wa kupambana na ajira za utotoni ili kuhakikisha watoto wanapata haki zao za msingi ikiwemo kupata Elimu.
Akijibu swali katika kikao cha baraza la wawakilishi kwa niaba ya Waziri,Naibu Waziri wa kazi,Uwezeshaji,Vijana,Wanawake na Watoto Shadia Muhammed Suleiman amesema kutokana na wananchi kuunga mkono juhudi za serikali katika kupiga vita ajira za utotoni serikali imefanikiwa kuwarejesha skuli Baadhi ya watoto waliokuwa wanajishughulisha na kazi hizo.
Hata hivyo amesema kutokana na baadhi ya wananchi kushindwa kudhibiti watoto wao kujiingiza na vikundi hatarishi ikiwemo ajira za utotoni wizara hiyo pia imeandaa mpango maalumu wa utoaji elimu ya kupambana na ajira hizo ili kuhakikisha watoto wanapatiwa haki zao za Msingi.
Kwa mujibu wa kauli za Wizara hiyo zaidi ya watoto  elfu tano wa Wilaya 11 za Zanzibar  waliokuwa wanajishughuliza na Ajira za utotoni wamerejeshwa skuli ili kuendelea na masomo yao.
 chanzo;zanzibar24.

Comments