Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar kulipa madai yote ya Walimu kwa awamu.

baraza-la-wawakilishiWizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar imesema inaendelea kufanya uchambuzi wa kina ili kuhakikisha inayapatia ufumbuzi matatizo yote yanayoikabili sekta ya elimu ikiwemo tatizo la uhaba wa walimu wa masomo mbalimbali.

Akijibu swali katika kikao cha baraza la wawakilishi huko chukwani Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mmanga Mjengo Mnawiri amesema kwa kipindi kirefu skuli za Zanzibar hususani Mkoa wa Mjini na za Shamba zinakabiliwa na tatizo hilo na kupelekea wanafunzi kukosa haki zao za msingi.

Katika kulipatia Ufumbuzi tatizo hilo Wizara inaendelea na hatua ya kuwaajiri walimu wa masomo ya Sayansi na hisabati pamoja na masomo ya kingereza,Historian a Jiografia ili kuondoa usumbufu wanaoupata wanafunzi wakati wanapohitaji elimu.

Wakati huo huo akijibu suali la nyongeza kuhusu mpangilio mbaya wa mishahara pamoja na  Posho wanazodai walimu kwa shughuli mbalimbali ikiwemo posho za likizo na kusainisha mitihani ya wanafunzi amefahamisha kuwa tatizo hilo limeanza kuchukuliwa hatua za awali ambapo walimu hao watalipwa kwa awamu.

chanzo;Zanzibar24

Comments