“Katibu wa chama wilaya huandika barua ya kuomba kibali cha kufanya
ziara na kuipeleka polisi, kilichotokea alimtumia katibu wa Jumuiya ya
Vijana CUF ambaye katiba haimruhusu na kwamba makatibu wa wilaya husika
wenye mamlaka walitoa taarifa polisi ya kutoitambua ziara yake,” amesema
na kuongeza.
“Polisi walipoona kuna mgongano wakazuia ziara kwa kuhofia fujo
walichokifanya ni kusitisha ili wakubaliane, jambo ambalo
hawakulifanya.”
Sakaya amedai kuwa”Katiba ya CUF ibara ya 96 kipengele cha 1 ukurasa
wa 87 inaeleza kuwa Naibu Katibu Mkuu ana mamlaka ya kuratibu ziara za
viongozi, sambamba na makatibu wa chama ngazi za wilaya ndio wenye
mamlaka ya kuratibu ziara za viongozi na ndio maana uongozi wa serikali
na vyombo vya dola hufanya maamuzi kwa kutumia katiba yetu,”
Amesema kilichotokea kwa Maalim Seif katika mikoa ya kusini, kitaendelea kutokea katika wilaya yoyote Tanzania Bara.
Novemba 19, Jeshi la polisi mkoani Mtwara lilizuia Mkutano wa ndani
wa Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad uliotarajiwa kufanyika
mkoani humo.
chanzo;zanzibar24.
Comments