Ndege iliyobeba watu 81 wakiwemo wachezaji wa klabu ya soka ya
Chapecoense kutoka Brazil imeanguka wakati ikikaribia kutua katika mji
wa Medellin nchini Colombia, mamlaka zathibitisha.
Taarifa kutoka eneo la tukio bado hazijakamilika ila zipo zinazosema kuwa kuna watu waliopona.
Maofisa
wa uwanja wa ndege wa Medellin wamesema wachezaji wa Chapecoense
waliokuwa kwenye ndege hiyo walikuwa safarini kwenda kucheza fainali ya
Copa Sudemericana dhidi ya Atletico Nacional ya Medellin, Colombia.
Kutokana na ajali hiyo, mechi baina ya timu hizo iliyokuwa ichezwe kesho imeahirishwa hadi itakapotangazwa tena.
chanzo;mpekuziblog.
Comments