Mama Mwanamwema Shein alitoa pongezi hizo huko
katika ukumbi wa Chuo cha Mafunzo ya Amali Vitongoji, Chake Chake Pemba
katika mkutano maalum kati yake na Wanachama na Viongozi wa Umoja wa
Wanawake Tanzania (UWT).
Katika hotuba yake Mama Shein, aliwapongeza akina mama hao kwa
kusimama kidete katika kuitumia haki yao hiyo bila ya woga na kusisitiza
kuwa ujasiri wao ni wa kupigiwa mfano.
Alisema kuwa kazi iloyopo mbele yao hivi sasa ni kuendeleza shughuli
za ujenzi wa wa nchi kwa kushirikiana na UWT na kuhakikisha kwamba
wanawake hawaachwi nyuma.
Mama Shein alitumia fursa hiyo kuwakumbusha wanawake na wananchi wote
kwa ujumla kuongeza bidii katika kuunga mkono juhudi za Serikali zenye
lengo la kuwawezesha wananchi kiuchumi, ili waweze kujiajiri wenyewe.
Alieleza kufarajika kwake kwa kuwepo mwamko mkubwa wa kuanzisha
vikundi vya Ushirika, SACCOS na kuongeza nguvu katika kilimo hasa cha
mboga mboga.
Katika mkutano huo Mama Shein aliwakabidhi kadi wanachama wapya 30 wa Jumuiya ya UWT wa katika Wilaya hiyo ya Mkoani.
Nae Mama Asha Balozi, Mke wa Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar,
aliwapongeza akina mama hao kwa juhudi walizozichukua katika kuhakikisha
chama chao cha CCM kinaendelea kuongoza huku akiwasisitiza wanajumuiya
hao kuwa kitu kimoja na kuondokana na ubinafsi.
Mapema Mama Fatma Karume, Mjane wa Marehemu Mzee Abeid Amani Karume
aliwataka akina mama wasirudi nyuma na badala yake wawe kitu kimoja na
washirikiane kama akina mama wenzao walivyoshiriki katika harakati za
kudai uhuru wa Zanzibar.
Nae Kaimu Katibu Mkuu, alitumia fursa hiyo kuwahamasisha akina mama
hao kuchukua fomu za kugombea nafasi mbali mbali za uongozi katika
Jumuiya hiyo katika uchaguzi ujao wa chama na kuwaeleza kuwa wanachama
wote wa chama hicho sifa za kuongoza.
Akiwahutubia viongozi na wanachama wa Jumuiya ya UWT, Wilaya ya Wete,
Mama Shein aliwaomba mashehe, walimu, wanasiaasa na wale wote wenye
nafasi za uongozi katika Taasisi na Jumuiya mbali mbali wasimame kidete
na kukemea vitendo vya udhalilishaji.
Alisema kuwa vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia na ukatili dhidi
ya wanawake na watoto bado vinaendelea kuriopotiwa katika Mkoa huo wa
Kaskazini Pemba pamoja na Mikoa yote ya Zanzibar.
Mama Shein alisisitiza kuwa vita dhidi ya vitendo hivyo havitoweza
kufanikiwa iwapo hawatochukua nafasi yao katikajamii kwa kuelimishana na
kuwaelimisha watoto juu ya madhara ya udhalilishaji kwa kila mmoja kwa
nafasi aliyonayo atakeleze wajibu wake.
Nao Viongozi wa UWT, Wilaya ya Wete walimpongeza Mama Shein kwa
utaratibu aliouchukua wa kwenda kuwashukuru na kuwapongeza akina mama
hao kwa kushiriki vyema katika uchaguzi mkuu uliopita ambao umeendelea
kuiweka CCM madarakani.
Viongozi hao walitunmia fursa hiyo kueleza baadhi ya changamoto
walizokumbana nazo ikiwa ni pamoja na kususiwa kuuziwa bidhaa, misiba,
harusi pamoja na kusisiwa katika masuala mengine ya kijamii.
Walimpongeza Dk. Shein kwa hatua anazozichukua za kusimamia mafisadi
pamoja na jinsi anavyotekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM huku wakieleza
kuwa umoja wao ndio ngao kubwa iliyosababisha kupatikana kwa ushindi
mkubwa wa uchaguzi uliopita katika Majimbo ya Wilaya na Mkoa huo.
Nae Waziri wa Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Vijana, Wanawake na Watoto
Maudline Castico aliwaeleza akina mama hao juhudi za Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar chini ya uongozi wa Dk. Shein katika kupambana na
vitendo vya unyanyasaji, jinsi inavyowasaidia wazee, vijana, pamoja na
wanawake na watoto.
chanzo; zanzibar24.
Comments