Mbatia ambaye pia ni Mbunge wa Vunjo, Mkoa wa Kilimanjaro alipelekwa
India Novemba 10 kwa matibabu ya mguu huo ambao umekuwa ukimsumbua muda
mrefu na alifanyiwa operesheni Novemba 14.
Akizungumza kwa simu kutoka India, Dk Baltazar Mbatia ambaye ni mdogo
wa mbunge huyo amesema kaka yake alifanyiwa upasuaji kuanzia saa
mbili asubuhi hadi saa sita mchana.“Wakati tunakuja hapa India, kaka
(Mbatia) alikuwa akilalamika sana juu ya maumivu aliyokuwa akiyapata
katika mguu wake.
Hata hivyo tunamshukuru Mungu sasa anaendelea vyema
baada ya upasuaji wa mafanikio kukamilika,” amesema huku akisisitiza
kuwa maadili ya udaktari hayaruhusu kusema kwa undani mgonjwa anaumwa
nini isipokuwa mhusika mwenyewe au mamlaka husika atakazoziagiza.“Kabla
ya kuzungumza na wewe, niliongea na Mheshimiwa (Mbatia) kaniambia
anaendelea vizuri na amewataka Watanzania kuendelea kumwombea,” amesema
Dk Mbatia.
Mkuu wa Kitengo cha Habari Elimu na Mawasiliano wa Bunge, Owen
Mwandumbya amesema Mbatia anatarajiwa kurudi Tanzania katikati ya wiki
ijayo baada ya matibabu yake kukamilika.
Chanzo:zanzibar24.
Comments