Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amesema hayo leo 22-Nov-2016
Jijini Dar es Salaam wakati akifungua mkutano wa mwaka wa kujadili
masuala ya gesi na mafuta barani Afrika ulioandaliwa na Kampuni ya
Getenergy ya
Uingereza.
Uingereza.
Katika hotuba yake, Makamu wa Rais amewahakikishia washiriki wa
mkutano huo kuwa Tanzania imeweka mazingira mazuri ya uwekezaji kwenye
sekta ya mafuta na gesi na itakuwa bega kwa bega na wadau wanaotaka
kuwekeza katika sekta hiyo ili kuhakikisha uwekezaji utakaofanyika
unakuwa na manufaa kwa pande zote mbili.
Amesisitiza kuwa kwa sasa Serikali ya Tanzania inaendelea na
mkakati kabambe wa kusomesha wataalamu wa fani ya mafuta na gesi ndani
na nje ya nchi ili kuhakikisha taifa linajitosheleza kwa wataalamu hao
ambao watakuwa na uwezo na ujuzi wa kufanya kazi kwa viwango
vinavyotakiwa katika sekta za gesi na mafuta.
Makamu wa Rais amesema Tanzania imegundua kiasi kikubwa na gesi na
ana imani kubwa kuwa mafuta nayo yanapatikana hivyo ni muhimu kwa
mataifa ya Afrika kujipanga kuwa na wataalamu wake wazalendo wa kutosha
watakaoshikiri katika uchumi wa gesi na mafuta kwa kuajiriwa kwenye
makampuni yanajihusisha na utafiti na
uchimbaji wa gesi na mafuta.
uchimbaji wa gesi na mafuta.
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amesema anaimani kubwa kuwa
rasilimali ya gesi na mafuta zitakagundulika na kuchimbwa barani Afrika
zitasaidia kwa kiasi kikubwa ukuaji wa uchumi wa mataifa hayo, uchumi
ambao utasaidia kuimarisha utoaji wa huduma bora za kijamii kwa
wananchi katika nchi husika.
Mkutano huo wa siku Mbili wa Kimataifa umekutanisha wadau
mbalimbali wa sekta ya gesi na mafuta kutoka ndani na nje ya nchi ambao
wanajadili kwa kina na kubadilishana uzoefu kuhusu njia bora za
uwekezaji katika sekta hiyo barani Afrika.
chanzo; zanzibar24.zanzibar24.
Comments