Amesema kiwanda hulazimika kusitisha uzalishaji wa sukari kutokana
na upungufu wa miwa na huku ikwalipa mishahara wafanyakazi bila ya
kuzalisha na kukipelekea kiwanda kuingia katika hasara.
Ameeleza hayo Ofisini kwake Mahonda wakati Kamati ya Fedha,
Biashara na Kilimo ya Baraza la Wawakilishi ilipofanya ziara ya
kutembelea kiwanda hicho kuangalia mafanikio na changamoto
zinazowakabili .
Bw Pronav Shah ameieleza Kamati hiyo ya Baraza la Wawakilishi kuwa
sehemu kubwa ya mashamba ya kiwanda imevamiwa na wananchi wa kawaida
kwa shughuli zao ikiwemo ujenzi wa nyumba huku wakijua kuwa ni sehemu
ya kiwanda na kupunguza ukubwa wa shamba hilo.
“Sehemu kubwa ya shamba la miwa hivi sasa limevamiwa na watu wa
kawaida na inasemekana wanaungwa mkono na baadhi ya viongozi wa shehia,”
amelalamika Meneja huyo.
Katika hatua nyengine Meneja huyo wa Biashara ameiomba serikali
kuwapatia bima ili inapotokea ajali waweze kufidiwa gharama za ajali
hiyo.
Amesema iwapo serikali itawapatia bima itawasaidia hasa kwa vile
mara kwa mara mashamba ya miwa hushambuliwa na moto ambao haujulikani
chanzo chake licha ya juhudi za uchunguzi zinazofanwa na jeshi la
Polisi.
Bw. Pronav Shah ameshauri kuruhusiwa kupanua soko la kuuza sukari
katika soko la Tanzania Bara ambalo hivi sasa bei ni tafauti na Zanzibar
ama kuuza sukari yao Zanzibar kwa bei ya soko la Tanzania Bara.
Nae mwenyekiti wa Kamati ya Fedha , Biashara na Kilimo Yussuf Hassan
ameutaka uongozi wa Kiwanda hicho kuendeleza uzalishaji wa sukari ili
kuwasaidia vijana kupata ajira na kufikia lengo la kujitosheleza kwa
bidhaa hiyo.
Ameuhakikishia uongozi wa kiwanda hicho kuwa ombi lao la kupata ardhi
zaidi kwa ajili ya kuongeza mashamba ya miwa watalifikisha katika ngazi
za juu ili liweze kupatiwa ufumbuzi.
Amesema Serikali inafahamu kuwa kufanikiwa kwa Kiwanda cha sukari cha
Mahonda itakuwa ni kivutio kwa wawekezaji wengine kuja kuwekeza
Zanzibar.
chanzo; zanzibar24.
Comments