Mwenyekiti huyo ametoa kauli hiyo baada ya mkuu huyo wa mkoa kufika
sokoni hapo kwaajili ya kusikiliza kero zinazowakabili wananchi ikiwa ni
siku ya nne ya ziara yake katika manispaa ya Temeke.
Unaweza ukadhani ni masihara lakini ndivyo hali halisi ilivyokuwa
baada ya mkuu wa mkoa wa Dar es salaam kutoa nafasi kwa wakazi wa Mbande
hususan wafanyabiashara wa soko hilo kutoa kero zao.
Kufuatia tuhuma hizo ikamlazimu mkuu wa mkoa kumsimamisha mwenyekiti
wa soko hilo Hassani ili kujibu tuhuma hizo ndipo alipotoa kauli hiyo na
kufafanua kuwa bei hiyo ya shilingi laki nne kwa kizimba ni makubaliano
kati yao na wananchi hao, pia fedha hizo zimetumika kwa ajili ya
kuendesha soko hilo, ambalo bado halijakabidhiwa kwa Halmashauri.
Kufuatia utetezi huo ikamlazimu Mkuu wa Mkoa kutumia busara ambapo
ameuagiza mkuu wa wilaya ya Temeke Felix Lyaniva kusimamia uundwaji wa
uongozi wa soko hilo haraka mpaka kufikia mwezi Desemba kero
zinazolikabili soko hilo ziwe zimetatuliwa.
chanzo; zanzibar24.
Comments