ZBS yawataka wafanyabiashara kufuata masharti ya kiafya.

zbsTasisi ya viwango Zanzibar (ZBS) imesema katika kuondoa tatizo la bidhaa zisizo na viwango nchini wafanya biashara hawana budi kufuata masharti ya kiafya yaliowekwa ili waende sambamaba na mahitaji ya watumiaji wa bidhaa hizo.
Akizungumza na Zanzibar24 Afisa uhusiano wa taasisi hiyo  Aisha abdul-kher Mohammed amesema baadhi ya wafanya biashara wamekuwa wakifanya biashara zao bila ya kuthibitisha na kuhakikiwa kwenye taasisi hiyo jambo ambalo ni kinyume na taratibu zilizowekwa.

Hata hivyo amesema katika kukabiliana na tatizo hilo wameandaa mfumo mpya wa utoaji elimu juu ya faida na hasara za kufanya biashra ilokosa kuthibitisha kisheria ili waweze kufika lengo la kuweza kudhibiti biadhaa zisizo kiwango kuenea Nchini.
Aidha ametowa wito kwa wanfanya biashara za ujasiria mali na waingizaji wa biashara kutoka nnje ya nchi kuwa na utaratibu wa kupeleka biashra zao ili kuweza kuuza biashra zisizo na madhra kwa watumiaji .
chanzo;Zanzibar24.

Comments